THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BALOZI ADADI AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI

MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini. Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini. 
Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya Muheza. “Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma kwa bidii “Alisema. 
Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na sera ya viwanda. “ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma kwa bidii “Alisema .
Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu ili kuona namna ya kulimaliza. 
Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo Julitha Akko 
Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini