THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

Na Othman Khamis Ame

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Chama cha Skauti Nchini kuongeza nguvu za kuwaelimisha Vijana wenzao hasa walioko Vijijini ili wajikomboe kupenda kujishughulisha na kazi au miradi ya ujasiri amali.
Alisema Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na vigenge vya kihuni mitaani vinavyopelekea kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya wizi pamoja na vitendo vya kudhalilisha watoto wanawake na watu wenye mahitaji Maalum.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Mkoani Dodoma kushiriki Tamasha la Wiki Moja la Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania hapo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Alisema zipo fursa nyingi za ajira zinazopatikana katika Sekta ya Utalii ambazo Vijana endapo wataamua kuzichangamkia zinaweza zikawapatia kipato kwa kutumia soko la bidhaa zinazotokana na kilimo cha mboga mboga na mazao ya Baharini.
Balozi alifahamisha kwamba Uskauti kwa vile hauna mafungamano ya itikadi ya Kisiasa wala Dini unalengo la kuwaunganisha Vijana katika harakati zao za kimaisha kupitia misingi ya kujenga Utaifa wao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa vijana wa Skauti kufundishwa mbinu na mafunzo ya kuogelea na kuzamia kutokana na majukumu yao yaliyowazuunguka ya kuwa wao ni miongoni mwa Taasisi zinazotoa huduma wakati yanapotokea maafa au majanga.
Balozi Seif alielezea kuridhika kwake na Kanuni 10 za Skauti zinazoelekeza uzalendo unaojenga Taifa lenye Wananchi wanaopendana na kuwa na nguvu za kukabiliana na changamoto zinazowazunguuka katika misingi ya nidhamu na uwajibikaji.
Mapema Kamishna Mkuu Msaidizi wa Chama cha Skauti Zanzibar Maalim Suleiman Takadir alisema Skauti iliasisiwa Zanzibar mnamo mwaka 1912 na Mwaka 1917 ikaanzishwa upande wa Tanzania na kufifia katika miaka ya 60.
Maalim Takadir alisema Chama hicho kilianzishwa tena Mwaka 1992 chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour ili kufufua ari ya kuwajenga Vijana katika uzalendo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akivishwa Skafu na Kijana Omar Amour Said wa Skauti nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar kabla ya kuzungumza na Vijana wa Chama cha Sakauti Zanzibar. Kati kati yao ni Raius wa Chama cha Skauti Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma.
Balozi Seif akiambatana na Rais wa Skauti Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma wakielekea ndani ya Ukumbi wa Mkutano kuzungumza na Vijana wa Skautio Zanzibar wanaotarajiwa kuondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Dodoma katika maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania.

Balozi Seif akimpongeza Kijana Kassim Yussuf Msoma Mashairi ghibu baada ya kughani kwenye Mkutano wa Skauti Zanzibar uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
Baadhi ya Skauti wa Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Chama hicho uliohutubiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uliokuwa wa matayarisho ya mwisho wa Vijana wake kujiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.
Baadhi ya Makatibu wa Skauti wa Mikoa ya Unguja wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif ambaye hayuko pichani hapo katika Ukumbi wa zamia wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwahutubia VBijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.Picha na – OMPR – ZNZ.