Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya Endsight iliyo chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Millenia la Marekani (MCC) imeazimia kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha miradi ya Maendeleo kupitia miundombinu ya Mawasiliano na huduma za Kijamii. 
Rais wa Taasisi hiyo Bwana Matthew McLean alitoa kauli hiyo wakati alipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. 
Mazungumzo hayo pia yalijumuisha Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usarifishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum pamoja na watendaji wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali. 
Bwana Matthew alisema Endsight imekuwa ikitoa ushauri wa Kitaalamu katika fani ya uhandisi katika kuona kiwango cha miundombinu kinachowekwa kwenye miradi inayohusika zaidi na masuala ya uhandisi inatekelezwa katika hadhi na daraja inayotakiwa kitaalamu. Alisema miundombinu ya bara bara na Mawasiliano, kilimo ikiwemo pia miradi ya huduma za maji safi na salama inahitaji ungalizi sahihi katika uanzishwaji wake ili wakati inapoanza kufanya kazi itoe huduma sahihi iliyokusudiwa kitaalamu. 
Naye Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib pamoja na watendaji wa Serikali walimueleza Bwana Matthew kwamba Zanzibar bado inakabiliwa na changamoto wa upatikanaji wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar akizungumza na Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi  ya Endsight  iliyo chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Milenia la Marekani (MCC)  Bwana Matthew McLean ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi Kati kati akiwa katika pamoja na Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi  ya Endsight  Bwana Matthew  McLean aliyeko upande wa Kulia yake , Waziri Ardhi Mh. Salama Aboud Talib Kushoto  yake, Naibu Waziri Ujenzi Mh. Mohamed Ahmed Salum wa Pili kutoka Kushoto pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...