Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa Jamii Nchini kuendelea kukuza maadili na kujiepusha na vitendo vya unyanyasi wa kijinsia dhidi ya Watoto na Wanawake ili irejeshea heshima yake Zanzibar. 
Alisema Visiwa vya Zanzibar havikuwa ni kituo muhimu cha Biashara katika mkarne zilizopita bali pia vilikuwa ni kitovu cha Elimu, heshima, ustaarabu na ukuzaji wa silka, mila na desturi za Utamaduni wa asili. 
Akilifungua Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari hapo katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michenzani Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwaomba wana Jamii kushirikiana na Wizara inayosimamia Utamaduni katika kuuenzi Utamaduni wa Taifa hasa kuhamasisha jamii kuepuka tabia zisizofaa zinazowadhalilisha Watoto, Wanawake na Watu wenye mahitaji Maalum. Balozi Seif alisema suala la kukuza utamaduni si jambo geni na ni vyema wazazi wa karne hii wakaiga mifano ya Wazazi wa zamani waliotumia mbinu mbali mbali zikiwemo sherehe za jando na unyago mfumo uliomtayarisha Kijana wa Kike na wa Kiume namna ya kukabiliana na maisha yake ya baadae. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia vitu vya sanaa za mkono wakati alipotembelea maonyesho ya Wajasiri Amali kabla ya kuzindua Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari.
 Balozi Seif  akihitaji maelezo kutoka kwa Mjasiri amali wa sanaa ya vitu vya ufinyanzi kwenye maonyesho ya kazi za sanaa katika uwanja wa Kumbu kumbu ya Mapinduzi Kisonge Michenzani Mjini Zanzibar.
 Mjasiri amali wa utengenezaji wa vitu vya  sanaa ya asili Viatu vya Mitarawanda kutoka Shehia ya Bweleo Bwana Ali Mwinjuma Kirobo akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea banda lao.
 Paredi la wasanii mbali mbali kutoka Wilaya za Unguja wakionyesha umahiri wao katika udumishaji wa Utamaduni wa Mzanzibari hapo Kisonge Mnara wa Kumbu kumbu.
Balozi Seif akionyesha umahiri wake katika kucheza ngoma ya ndege kutoka Skuli ya Msingi Kisiwandui iliyokuwa ikitumbuiza kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari hapo Mnara wa kumbu kumbu Michenzani Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...