Msanii wa muziki wa asili ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Mrisho Mpoto ametangaza deal kwa waimbaji pamoja na wapiga ala za muziki kujitokeza kwa wingi Sabasaba jijini Dar es salaam katika banda la maonyesho la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kupata wasanii wapya watakao unda bendi mpya ya hifadhi hiyo.
Akiongea wa wadau waliojitokeza kwa wingi katika banda hilo, Mrisho Mpoto ambaye ni balozi wa hifadhi hiyo, alisema vijana hao wanatakiwa kujua kuimba pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vitu vinavyopatikana.
“Hii fursa kwa waimbaji wa muziki pamoja na wapiga ala za muziki, tunatakiwa kuanzisha bendi ya muziki ‘Ngorongoro Band’, kuandaa nyimbo maalum ambazo zitakuwa zinawaelimisha watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hii. Kuandaa wimbo ambazo zitawafanya watanzania kuijua zaidi mbuga zao , masuala ya utalii pamoja na vitu mbalimbali vilivyomo ndani yake,” alisema Mpoto.
Katika hatua nyingine Mrisho amesema anashukuru wadau mbalimbali wanajitokeza kwa wingi katika banda la Ngorongoro kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wanyama wanaopatika.
“Kuwema kweli mambo yamekuwa mazuri sana katika banda letu, watu wanakuja kwa wingi sana kwa sababu sisi tunatoa burudani na elimu, burudani na elimu, kuna bendi hapa In African ambio inatoa burudani kila siku, kuna mastaa mbalimbali wanakuja kutoa burudani kama mlivyowana akina Stara Thomas, Solid Ground, Steve B&B na wengine wengi ambao wanakuja na kuondoka. Kwa hiyo kikubwa zaidi kwetu ni burudani na elimu,” alisema Mpoto.
Aliongeza, “Pia tumekuwa na kipengele cha elimu kuhusu wanyama kila siku na baada ya haps tunawaita watoto waeleze vitu ambavyo wanajifunza kila siku na tumekuwa tukitoa zawadi ya mpaka tsh milioni moja kwa siku na tumeona matunda kabisa watoto wanakuja hapa hawajuhi chochote lakini wakiondoka hapa wanaweza kueleza vitu mbalimbali ambavyo vinapatika katika hifadhi ya Ngorongoro,”
Mshairi huyo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda hili pamoja na watoto wao ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...