Benki ya KCB Tanzania inaendelea kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa 2jiajiri. 

Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB 2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.

KCB 2jiajiri ni programu inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji, utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.

“Programu hii ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.

Akielezea kuhusiana na programu ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu darasani, kwa sasa wananufaika kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka kwa washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.
Afisa Sheria Bi. Doris Mugarula (wakwaza kushoto) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea maendeleo ya biashara yake ya nguo mkoani Arusha. 
Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (wakwanza kulia) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa Ally (kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani Morogoro.
Afisa Masoko, wa Benki ya KCB, Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani Morogoro.
Afisa Masoko Bi. Ghati Muhere (aliyechuchumaa) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth (aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Masoko, Bi. Ghati Muhere (wakwanza kulia), Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (watatu kushoto) na Afisa Fedha, Bi Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Mercy (wakwanza kushoto) katika biashara yake ya huduma za Interneti mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...