Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kushirikiana na Tanzania kujenga mradi mkubwa wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kuipatia mkopo wenye masharti nafuu. 

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji. 

Dkt. Weggoro amesema kuwa Benki yake imeridhika na utendajikazi wa Serikali ya Awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na hivyo kuifanya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo kukubali kufanikisha ujenzi wa Reli hiyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi. 

Amesema kuwa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa ni muhimu kwa uchumi wa Taifa lakini pia kwa uchumi wa nchi za Maziwa Makuu kwa kuunganisha nchi kama vile Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na baadae itaunganishwa na Reli ya Kaskazini upande wa Kenya. 

“Benki iko tayari na inasubiri Tanzania ilete mapendekezo ama maombi ili yafanyiwekazi, tutakaa pamoja ili tuone Benki itasaidia kiasi gani na Benki pia inaweza kuwatafuta wadau wengine tunaosaidiana nao katika miradi mikubwa kama hii” Aliongeza Dkt. Weggoro
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro kuhusu ushirikiano mzuri na Benki hiyo katika Maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipokutana naye ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), akiishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, kwa namna inavyoshirikiana na Tanzania kukuza uchumi wake, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza namna Benki yake itakavyofadhili ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwando cha Kimataifa (Standard gauge) pamoja na kuhuisha Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania-TANESCO, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, anayehudumia Kanda ya Afrika, Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) akimwonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), zawadi ya picha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao, Jijini, Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...