THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BREAKING NEWZZZZ: Wahalifu wengine wawili wauawa tena IKWIRIRI, mmoja atambulika.

Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili  wanaosadikiwa kuwa  ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika  Kanda maalumu ya  kipolisi Rufiji ambapo  mmoja  kati ya watu hao  ametambulika  kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki  kwake katika matukio ya  mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.
Akielezea tukio hilo,  Mkuu wa Operesheni Maalum  za Jeshi la Polisi,  Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la  Utende kata ya Ikwiriri,  wilaya Rufiji kanda maalum  ya Polisi  Rufiji.

 “Askari  Polisi  wa doria  waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walipoanza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia  askari kwa risasi. Askari nao kwa ujasiri walijibu   mashambulizi na kufanikiwa  kuwajeruhi  wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye  walifariki  wakipelekwa Hospitali  ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza kuwa  katika eneo  hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo  ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2).  Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.
 Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba  opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji  ni endelevu  na hakuna atakayebaki.