Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake wanne waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA)  kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.
Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo  iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya  (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya (51).

Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema (31),  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.

Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki (pichani kulia) na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.
-----  ------  --------

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...