Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa kosa la kutoa kauli za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla.

Hapi ameagiza mbunge huyo kukamatwa, kukaa korokoroni kwa saa 48, kuhojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa maneno aliyoyatoa jana akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema mtaa wa ufipa. 

Hapi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Mdee ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi unaoweza kuhatarisha amani na utulivu.
"Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mh. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu."
Alisema DC Hapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nafikiri kuna matatizo ya kujipima nguvu kati ya jamaa hawa na wabunge. Itatuletea ukorofi

    ReplyDelete
  2. Nimesikiliza hotuba ya Mbunge Halima Mdee. Amejenga hoja, akinukuu mikataba na makubaliano mbali mbali. Mkuu wa wilaya kama ana jambo, alete hoja zake, kupinga hoja za mbunge. Ninaamini wa-Tanzania ni watu wenye akili, ambao wanaweza kubaini ukweli uko wapi. Siafiki uamuzi wa mkuu wa wilaya kutumia mabavu dhidi ya mbunge huyu. Tujenge utamaduni wa kukosoa hoja na kujibu hoja kwa hoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...