Na Dotto Mwaibale
KAMPENI ya Castle lite unlocks inahamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania.
Wito huo umetolewa na Meneja wa mahusiano ya wateja wa kampuni ya Tanzania Brewaries Limited (TBL) kwa Afrika Mashariki, George kavishe katika taarika yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo alitumia fursa kuwataja wadhamini na wabia wa kampeni hiyo. 
“Kwa mara nyingine tena tunawakumbusha wapenzi wa muziki, hasa walioko katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu kujiandikisha kwa wingi kwani tukio hilo la aina yake linakaribia” alisema Kavishe, akiongeza kuwa washiriki watapata fursa adimu sana ya kufurahia bonanza lamuziki litakalo tayarishwa na brand ya kipekee ya bia, Castle Lite hivi karibuni.
Akitangaza washirika, kavishe alipongeza mchango wao, akisema kwamba wametekeleza jukumu kubwa katika mafanikio ambayo kampeni hiyo imefikia mpaka sasa.
Alitaja wadhamini kama vile Tigo Tanzania (mshirika  rasmi wa mawasiliano ya Simu), Clauds FM (Mshirika kama chombo cha habari), CFAO Motors  (Mshirika katika usafirishaji), Marlborona Serena Hotel Dar es Salaam (Mshirika katika malazi).
“Tunawashukuru sana washirika wetu kwa kukamilisha juhudi zetu katika kuelekea kwenye tamasha la nne la muzikiambalo linahakika kuwa litakuwa ni chanzo cha mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki wa wandani”, Kavishe amesema kuhusu Bonanza kubwa ambalo limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezihuu wa julai katika ukumbi wa Leader’s Club hapa Dar es salaam. 
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuhamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David na Meneja Masoko wa TBLKitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.


Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Masoko kutoka Kampuni ya CFAO Motors Ltd, Angelina Ndege akizungumza katika mkutano huo kuhusu kudhamini tamasha hilo.
Wasanii wa hapa nchini watakaotoa burudani katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Vanessa Mdee, Nahreel Mkono na Aika Marealle.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...