Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha na barabara ya kutoka Furahisha hadi Pasiansi yenye urefu wa KM 2.7, imekamilka kwa asilimia 99 Mkoani Mwanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujezi wa daraja hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani humo na kuridhishwa na ukamilishwaji wa ujenzi wake. “Daraja hili litaondoa changamoto kwa wananchi wanaotembea kwa miguu na litapunguza au kuondoa adha ya msongamano wanaovuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine”, amesema Prof. Mbarawa. 

Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutunza daraja hilo na miundombinu yake ili liweze kutumika kwa muda mrefu kwani limekuwa nembo ya Mkoa wa Mwanza. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kujenga Daraja la Furahisha kwa kuwa limebadilisha mandhari ya Jiji hilo. “Jiji la Mwanza ni kitovu cha Kanda ya Ziwa, wananchi wameguswa moja kwa moja na mradi wa ujenzi wa daraja hili”, amesema Bw. Mongela. 


Muonekano wa daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha, mkoani Mwanza. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 na limejengwa na kampuni ya Nyanza Roads Works. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela (kulia), wakishuka ngazi za daraja la waenda kwa miguu lililojengwa eneo la Furahisha, alipokagua ujenzi wake mkoani Mwanza. 
Mhandisi Mkazi anayesimamia uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza Bw. Geofrey Asulumenye, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, upanuzi wa njia za kurukia ndege katika kiwanja hicho mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi Bw. Geofrey Asulumenye (kulia), kuhusu uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza, alipokuwa akikagua uwanja huo. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...