Serikali kupitia Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Rukwa imekamilisha ahadi yake kwa wananchi ya kuwapunguzia changamoto ya usafirishaji wa abiria na mzigio kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la mto Kalambo pamoja na barabara ya Sumbawanga Matai hadi Kasanga port (112km) ambapo Kilomita 71.4 zimeshawekwa lami.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja na barabara hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa Rukwa na nchi nyingine za jirani ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.

“Tuliwaahidi wananchi kujenga darala na barabara hii ili wafanyabiashara na wakulima waweze kusafirisha bidhaa na mazao yao kwenda katika masoko kwa wakati na hivyo kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla,” ameaema Eng. Ngonyani.

Ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali itahakikisha ndani ya kipindi cha miaka mitano inakamilisha ahadi zote walizoahidi kwa wananchi ili wananchi wanufaike na Serikali yao.

“Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ipo kwa ajili ya wananchi wote, na sisi kama wasimamizi tuliopewa dhamana kwenye Wizara tutahakikisha kile tulichokiahidi kwa wananchi tunakitekeleza kwa wakati ili wananchi wanufaike na uchumi wa nchi ukue,” amesisitiza Eng. Ngonyani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga Kituo cha Mzani cha Singiwe Kilichopo katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (112KM) Mkoani Rukwa wakati alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) akipanda katika Daraja la Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akikagua Daraja la Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika.Wa kwanza ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Rukwa Eng. Msuka Mkina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...