THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DC HAPI ASHUSHA PRESHA KWA WANANCHI KUNDUCHI, AHITIMISHA MGOGORO WA ARDHI WA MUDA MREFU

Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi leo ametangaza msimamo wa serikali ya wilaya ya Kinondoni kuwa wananchi wa Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi waliokuwa na hofu ya kuondolewa kuwa hawataondolewa na kwamba badala yake makazi yao yatapimiwa viwanja na watamilikishwa rasmi. 

Uamuzi huo umekuja baada ya mvutano wa miaka mingi baina ya manispaa ya Kinondoni na wananchi hao waliovamia eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya machimbo ya kokoto. Katika mvutano huo ulioibua kesi mbili zilizoendeshwa kwa muda mrefu na hatimaye manispaa kushinda kesi hizo, uamuzi umefikiwa kuwa Manispaa ya Kinondoni haitawavunjia na kuwaondoa wananchi hao wapatao zaidi ya 3000 waliojenga eneo hilo.
 Badala yake eneo hilo litapimwa ili kupanga vema mji na kuruhusu maeneo ya huduma za msingi za jamii kama barabara, shule, afya na zahanati kutengewa maeneo.
DC Hapi ameagiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kukaa maeneo hayo baada ya leseni ya uchimbaji kokoto eneo hilo kufutwa kutokana na uharibifu wa miundombinu.
"Hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi 3000, tutawapeleka wapi, kwani wao siyo wanakinondoni, kwani wao siyo watanzania" Alisema DC Hapi.
DC Hapi ametoa maagizo kwa watendaji kuhakikisha kuwa wananchi hao wanamilikishwa maeneo hayo kwao kufuata taratibu na sheria ambapo itabidi maeneo hayo yapimwe na wananchi hao wawe wavumilivu maana kuna baadhi ya maeneo yatatengwa kwa huduma za kijamii, ikiwemo vituo vya Afya, Polisi na barabara.
Hata hivyo DC Hapi amewatoa hofu wananchi wa maeneo hayo kuhusu kulipia gharama za upimaji wa ardhi ambazo itabidi wachangie, huku akieleza kuwa wataiandikia barua mamlaka ya chuo cha Ardhi ili waweze kutoa baadhi ya wanafunzi ambao watafanya upimaji katika eneo hilo bure na kuwaondolea wananchi gharama za ziada.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesisitiza kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na wananchi wanyonge kuhakikisha haki yao haipotei, huku Diwani wa Kata hiyo akihimiza ushirikiano katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayana chama, hvyo ni vyema kuondoa itikadi.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi akishangiliwa na wananchi mara  baada ya kuzungumza nao na kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi ambao hapo mwanza ilidaiwa na Manispaa ya Kinondoni kuwa wamevamia kwakuwa eneo hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Machimbo ya Kokoto.