Na Ofisa Habari Mufindi
Serikali Wilayani Mufindi, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kujitolea ya Jeshi la kujenga Taifa JKT kikosi cha 841 Mafinga, kuwa walinzi namba moja wa amani katika jamii zao, kwa kuwafichua waharifu watakao jaribu kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini kwa sasa .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kutoka kikosi cha 841 kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
 “ kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na maadui wa nje na ndani ya nchi wanaojaribu kuvunja Amani na utulivu uliostawi kwa muda mrefu hapa nchini, hivyo, nawaagiza  Mkalinde  kiapo chenu cha utii nauadilifu kwa Taifa na Mkuu wa nchi kwa kutekeleza sera ya Taifa inayotanabaisha kuwa  kila raia wa Tanzania ni Mlinzi wa nchi yake”
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewaasa vijana watakao pata fursa ya kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya kuhitimu mafunzo, wakafanye kazi kwa nidhamu, uadilifu na uaminifu na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuajiri vijana wa JKT pekee kwenye sekta zote zinazohusika na ulinzi na usalama wa nchi.
Jumla ya vijana (846) wavulana wakiwa (612 ) na wasichana (234) wenye elimu za Msingi mpaka chuo kikuu, wamehitumu mafunzo ya awali ya kijeshi ya miezi (06) na kufuzu kuingia hatua ya pili ya mafunzo ya Malezi na stadi za kazi katika Jeshi la kujenga Taifa JKT.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akitunuku zawadi kwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vizuri wakati wa mafunzo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe, akiwasili kwenye Ofisi za kambi ya 841 Mafinga kushiriki mahafali hayo
Vijana wa JKT wanaohitimu mafunzo ya awali, wakipita mbele ya Mgeni wa heshima kutoa heshima ya kijeshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...