Matiro amesema anasikitishwa na wananchi mjini Shinyanga kuwa wa kwanza kuchanga michango ya harusi na wengine kutumia pesa hovyo kwenye vileo na wakati kuna watoto wanahitaji msaada hata wa sare za shule na viatu ili waende shule lakini kutokana na kuishi mazingira magumu watoto wanakwama na hatimaye kufanya vibaya darasani. 

Matiro ametoa rai hiyo leo Alhamis Julai 6,2017 mjini Shinyanga wakati akikabidhi nguzo za shule kwa watoto 164 kati ya 1400 ambao wanaishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga. 

Matiro ametoa msaada huo kwa kwshirikiana na Shirika la TVMC na PWWCO ambayo yanasaidia watoto na akina mama wanaoishi katika mazingira magumu mjini Shinyanga. 

Matiro alisema lengo kuu la msaada huo kuuonesha umma kuguswa namna ya kusaidia watoto wanaoishi mazingira hayo na siyo kuiachia serikali peke yake zikiwamo NGO's na Wageni kutoka nje ya nchi kuja kuokoa watoto hao na wakati wananchi nao wana uwezo wa kuwatatulia changamoto hizo. 

"Ukipita mchango wa harusi unakuta watu wanakuwa wa kwanza kuchangia tena kwa haraka lakini likija suala la kusaidia watoto wanaoishi mazingira magumu, kila mtu utasikia akisema hana pesa ,wananchi mnatakiwa mbadilike" alisema Matiro. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wakazi wa mjini Shinyanga kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata elimu wakiwa katika mazingira rafiki na kupata ufaulu mzuri ambao utawafanya wafikie malengo yao ya maisha. 
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC mjini Shinyanga Mussa Jonas Ngangala akisoma taarifa kwa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jinsi shirika hilo linavyosaidia watoto wanaoishi katika mazingira Magumu na malengo yao juu ya kusaidia watoto 1,400 wanaoishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukabidhi sare za shule likiendelea 
Watoto 164 wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wamekaa wakisubiri kupewa msaada wa sare za shule na mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...