Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tabora imeendesha oporesheni ya kung’oa mazao mbalimbali ya bustani yaliyokuwa yamepandwa na wavamizi katika maeneo ya vyanzo vya maji na kando kando ya Bwawa la Igome na hivyo kusababisha uzalishaji wa maji kupungua.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi iliendesha zoezi hilo jana mjini hapa baada ya kugunduliwa kuwepo kundi kubwa la watu wanaondeshea kilimo cha mazao mbalimabli ikiwemo matunda na kuhatarisha afya ya watumiaji.
Katika oporesheni hiyo mazao mbalimbali kama vile majani ya maboga, hoho, nyanya na matembele yaliweza kung’olewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi alisema kuwa wavamizi hao wakiendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo vya Bwawa hilo ikiwemo kilimo cha mboga mboga na wakati mwingine wamekuwa wakiweka dawa ambazo wakati mwingine dawa hizo zimekuwa zikiingia katika maji hayo ambayo ndio wakazi wengi wa Wilaya ya Tabora wanatumia.
Mwalimu Mlozi aliongeza kuwa endapo maji hayo yasipowekewa dawa vizuri ya kusafisha upo uwezekano wa watumiaji kunywa dawa na kilimo zilizotoririkia majini.Aliongeza kuwa hali ya maji katika Bwawa hilo sio nzuri na endapo wavamizi hao wasipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Tabora kukabiliwa na upungufu wa maji katika miezi ijayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (aliyeshika miche ya nyanya) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani waliovamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (wa kwanza kushoto) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani walivamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo. Zoezi hilo lilifanyika jana katika eneo la Bwawa hilo.
Picha na Tiganya Vincent-RS  - Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...