Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla ahimiza watumishi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia sheria, miongozo,  taratibu na maelekezo yao ya kazi.

Akiwa katika ziara hiyo Mkoani Mtwara, alielekeza watumishi hao kuwa dhamana waliyopewa kuwahudumia wananchi wenzao ni kubwa hivyo hawana budi kuzingatia kanuni za Afya ili kuepuka maambukizi yatakayotokana na uzembe .

Aliwataka kulipa kipaumbele suala la usafi wa mazingira, vifaa na maeneo yote wanayofanyia kazi hususan uhifadhi wa taka za hospitali katika utaratibu maalum unaozingatia  mfumo wa kinga na udhibiti wa taka  (Infection Prevention and Control) .

Miongoni mwa mambo mengine aliyoyabaini katika ziara hiyo ni ubovu wa baadhi ya vifaa tiba katika maabara na vyumba vya upasuaji na kuagiza katibu mkuu wizara ya Afya kuchunguza mikataba yote ya usambazaji vifaa tiba na matengenezo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi na wa Hospitali ya Wilaya ya Masasi-Mkoamaindo (Hawapo pichani). Wengine anayemfuatia ni Mbunge wa Jimbo la Masasi  Mh. Abdalla Chuachua na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msasi. 
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kitanda maalum cha upasuaji alichokikuta katika hyali ya kutoridhisha kiafya.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua mambo mbalimbali ya kiutendaji katikaa hospitali hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...