Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi leo ampokea madawati 2579 kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Akipokea madawati hayo yaliyosafirishwa katika magari 19 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Dkt Nchimbi amelipongeza jeshi hilo kwa uzalendo huo wa kuhakikisha mali za umma zinafika Singida kwa ajili ya kuanza kusambazwa katika halmashauri husika zikiwa salama na katika hali nzuri.

Dkt Nchimbi amelipongeza Bunge kwa uzalendo wa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka nchini  ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda. 

Amesema madawati hayo yataongeza motisha kwa wanafunzi kujisomea kwakuwa mazingira yatawawezesha kuandika na kusoma kwa ufanisi zaidi.
Aidha Dkt Nchimbi amezitaka halmashauri zitakazopokea madawati hayo kuhakikisha wanayatunza ili yadumu na kuwanufaisha wanafunzi kwa muda unaostahili.

“Madawati na yenyewe yanahitaji ukarabati, sio kwakuwa mmepewa basi muyaache tu, hapana, ukiona ubao unalegea kidogo basi hakikisha unarekebisha na sio kuanza kusubiri waliotupatia ndo waturekebishie”, amesema na kuongeza kuwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipokea kwa furaha moja ya magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyokuwa yamebeba Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Madawati hayo yametolewa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimpongeza kwa furaha mmoja wa mwanajeshi aliyehusika kusafirisha Madawati 2579 yaliyotolewa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Madawati hayo yamefikishwa Singida kwa ajili ya urahisi wa kuyasambaza katika mikoa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishirikiana na wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Askari wa Magereza kushusha madawati yalitolewa na Bunge. Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...