Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kushoto), akitoa pongezi zake kwa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo Mfuko huo kwa ushirikiano na wabia wengine, umewekeza kwenye miradi mikubwa ya Mkulazi mkoani Morogoro na ule wa uboreshaji wa kiwanda cha viatu Karanga na ujenzi wa kiwanda kipya cha viatu kwenye eneo hilo kwa ubia na Magereza. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele akiwa na wafanyakazi wenzake.

(K-VIS BLOG/Khalfan Said)

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alitembelea banda hilo na kuipongeza PPF kwa uamuzi wake wa kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kujenga uchumi wa viwanda. Akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, utekelezaji wa miradi unaendelea vizuri kwa upande wa Mkulazi mkoani Morogoro na kiwanda cha viatu Karanga mjini Moshi ambacho kinaendeshwa kwa ubia na Jeshi la Magereza. 

Ukarabati wa kiwanda cha sasa unaendelea na unategemea baada ya kuweka mitambo mipya uzalishaji utaongezeka kutoka jozi 150 za viatu hadi kufikia jozi 400 kwa siku, alisema Bi. Mengele. "Uboreshaji wa kiwanda hiki cha ngozi sio tu utaongeza uzalishaji bali pia tunakusudia kununua malighafi za ndani na pia tutakuwa tumeongeza ajira." Alifafanua Bi. Mengele. 

Kwa upande wake, Waziri Dkt. Mpango ambaye alipata fursa ya kutembelea maeneo amabayo PPF imewekeza kwenye viwanda, alisema "Ninyi ni watu wazuri na niwapongeze kwa uamuzi wenu mzuri wa kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano ambayo tumejikita katika kujenga uchumi wa viwanda " Alisema Dkt. Mpango. Wakati huo huo Waziri Dkt. Philip Mpango, amewahimiza vijana kujiunga na PPF kupitia Mpango wake wa Wote Scheme, kwani kuna faida nyingi ambazo mwanachama aliyejiunga na Mpango huo atafaidika nazo. 

Dkt. Mpango alitoa rai hiyo wakati akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia Mpango wa "Wote Scheme", kijana wa miaka 18, Msuya S. Mageta, kwenye banda la Mfuko huo.

Dkt. Mpango alifurahishwa na uamuzi wa kijana huyo na kuwataka vijana wengine kuiga mfano wake. Pia aliipongeza PPF kwa huduma zake za haraka baada ya kushuhudia mwanachama wa PPF akichangia michango kupitia simu yake ya kiganjani kwenye banda la Mfuko huo. Waziri alitoa rai kwa wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani umepata mafanikio makubwa kwa kuweza kupata cheti cha ubora wa kimataifa kwa kutoa huduma bora zenye kiwango cha kimataifa (ISO 9001;2015) ambapo ndio Mfuko pekee wa Hifadhi ya Jamii kupata hati hiyo.



Waziri Dkt. Mpango, akimpongeza Bw.Sukulu Mageta, ambaye ni mzazi wa Msuya Mageta, (katikati), kijana wa miaka 18 aliyeamua kwa hiari yake kujiunga na mpango wa Wote Scheme.

Meneja Elimu kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi mkoba wenye vipeperushi vya taarifa za PPF, Waziri Dkt. Mpango.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...