Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib na kulia ni Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika kupambana na kadhia hiyo. 

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19 iliyokuwa nayo mara tu baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1996. 

Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa wananchi wanaeleza kwamba, miongoni mwa changamoto zinazosababisha msongamano ni kuwa benki za hapa nchini bado haziendani na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika sekta ya fedha. 

Alieleza kuwa katika Siku ya Sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi, mwaka huu yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Unguja, Wafanyakazi walipendekeza kuwa Serikali ikae na uongozi wa benki mbali mbali ili ione namna ya kupunguza kero hii kubwa ya msongamano na kuchelewa kutolewa huduma, hasa ifikapo mwisho wa mwezi. 

“Leo nimeona ni busara nikuleteeni mawazo hayo ya wafanyakazi, ambao pia, ni baadhi ya wateja wa benki zenu. Wahenga wanasema ‘Mjumbe hauawi’ ndio maana na mimi nimeufikisha ujumbe kama nilivyoambiwa”, alisema Dk. Shen. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akihutubia katika hafya ya ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (wa pili kushoto) pamoja na Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza katika hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wakati wa hafya ya ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati), Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar, Salama Aboud Talib (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (kushoto) pamoja na Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (aliyeketi nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja katika madawati na baadhi ya wanafunzi wa skuli ya msingi Madunghe ya Chakecaheke kisiwani Pemba. Madawati hayo yametolea na Benki ya CRDB kwa shule hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...