THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DOKTA MPANGO AKUNWA NA MWITIKIO WA WANANCHI KULIPA KODI

Na Benny Mwaipaja, WFM 
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewapongeza Watanzania nchini kote kwa mwitikio wao mkubwa wa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo kwa hiari, hatua ambayo itaiongezea Serikali uwezo wa kuwahudumia kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa pamoja na kuwahimiza wananchi kudai risiti wanapofanya manunuzi halkadhalika wafanyabiashara kutoa risiti wanapouza bidhaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi waliofurika kulipa kodi mbalimbali hususan za majengo katika viwanja hivyo vya Sabasaba, wameeleza kuwa mwitikio na hamasa kubwa waliyonayo ya kulipa kodi inatokana na imani yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano jinsi inavyosimamia maendeleo ya nchi kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wake Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi Bi. Honesta Nduguru, amewataka Watanzania popote walipo kutumia muda mfupi wa nyongeza uliobaki kulipa kodi badala ya kusubiri dakika za lala salama.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo toka kwa Bi. Honesta Ndunguru, Meneja Huduma kwa Mlipakodi, wa TRA alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.