Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
 Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa. 
Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC). Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women's Bank, Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...