Na Anil Ricco, Globu ya Jamii
Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL) inatarajiwa kuingia nchini Tanzania, July 12 kucheza Mchezo wake wa Kirafiki na Klabu ya Soka ya Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Everton inaingia nchini ikiwa na Gwiji wake wa Soka, Wayne Rooney aliyesajiliwa hivi karibuni.

Katika mchezo huo baina ya Everton na Gor Mahia, Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo, Yusuph Omary Singo amesema kuwa Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akithibitisha ujio wa Kikosi hicho, Mkurugenzi wa SportPesa nchini Tanzania, Abbas Talimba amesema maandalizi yote yamekamilika kwa Everton kutua nchini, amesema Kikosi hicho kinakuja na Wanandinga wake wote.

Kwa upande wa Upatikanaji wa Tiketi, Selcom kupitia Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo, Galusi Lunyeta amesema watu watakaokuja kushuhudia mchezo huo watahakikisha wote wanapata tiketi kupitia Mfumo huo wa Selcom, kuanzia saa mbili asubuhi siku ya Mechi.

Pia katika Suala la Ulinzi na Usalama, Inspekta wa Jeshi la Polisi, Hasheem Abdallah amesema kuwa njia zitakazotumika kuingia Uwanjani siku ya Mchezo huo katika Uwanja wa Taifa ni Mandela Road na Kilwa Road, watu kufika Uwanjani na kutoka.
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omary Singo akizungumza kwa niaba ya Serikali katika kuupokea ugeni wa Timu ya Everton wanaokuja kucheza Mchezo wa Kirafiki na Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa SportPesa nchini, Abbas Talimba akifafanua jambo juu ya ujio wa Timu ya Everton ya Uingereza July 12 mwaka
 Afisa Usalama wa TFF na FIFA, Inspekta Hasheem Abdallah akifafanua kuhusu Ulinzi katika Mchezo huo utakaopigwa July 13 katika Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo - SELCOM, Galusi Lunyeta akifafanua juu ya upatikanaji wa Tiketi siku ya Mchezo huo July 13.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...