THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Hali ya Yusuf Manji bado tete, kesi yake yapigwa kalenda hadi mwezi ujao
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa Mfanyabiashara  Yusufali Manji (41) bado anaumwa na yuko kwenye matibabu katika hospitali ya gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salam.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Bw. Nassoro Katuga amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.
Amedai kuwa, kesi hiyo leo ilikuja kwa kutajwa lakini Upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 4, mwaka huu.

Katika kesi hiyo Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa.
Katika Mashtaka hayo, wanadaiwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya milioni 195.5 na mihuri ya JWTZ na magari ya serikali kinyume cha sheria.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya Quality Group Deogratius Kisinda(28), mtunza stoo Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43) mkazi wa Chanika.


Mfanyabiashara  Yusufali Manji