HALMASHAURI ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wote watakaokwamisha upatikanaji wa majibu ya hoja za ukaguzi kwa muda waliokubaliana na hivyo kusababisha Halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka au hati chafu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Peter Onesmo alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano maalumu wa baraza la madiwani wa Halmashauri kupitia hoja za ukaguzi wa CAG kwa mwaka 2015/2016 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo mjini Igunga.

“Na kama taarifa hiyo itakuja kwamba hatua hazijachukuliwa hatutasita kuwachukulia hatua wale ambao wametusababisha tuvuke ile tarehe tuliyoweka utekelezaji hatujauweka,kwa hiyo kama mtu atakuwa anajitakia hayo basi afike tu huko apime”alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo hata hivyo alifafanua kuwa maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa huo kwamba watumishi wote wale watakaosababisha Halmashauri kuingia katika mahali kusikostahili,ni lazima watachukuliwa hatua za kisheria.

Akifungua mkutano huo maalumu,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanry alisisitiza kwamba watu pekee wenye mamlaka na madaraka ya kufanya maamuzi katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga ni watu wanaoitwa Baraza la madiwani kutokana na wao kuwa ndiyo wawakilishi wa wananchi.

“Kwa nini leo kuna districk Commisioner na Region Commishiner hapa,Regional Comisioner na district Comisioner wanakuja hapa kama wawakilishi wa Rais kwa maneno mengine ni wawakilishi wa serikali,kwa nini kwa sababu Halmashauri ya wilaya ya Igunga inapokea ruzuku ya serikali”alifafanua Mwananry.

Hata hivyo Mkaguzi wa nje,Mohamed Msangi aliweka bayana kwamba bado utekelezaji wa maoni ya CAG siyo wa kuridhisha kwani kati ya hoja 120 zilizotolewa kwa hesabu za mwaka 2015/2016 zikijumulisha na hoja za miaka ya nyuma,ni hoja 72 tu zilizopatiwa majinu ya kuridhisha na kufungwa na hivyo hoja 48 sawa na asilimia 40 zimeendelea kusalia.
Ni Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano maalumu wa Baraza hilo kupitia taarifa CAG.(Picha Na.Jumbe Ismailly)  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...