THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

HOSPITALI YA SHALBY YA NCHINI INDIA YAADHIMISHA MIAKA 15 YA KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI NCHINI.

Hospitali ya nchini India ya Shalby imesherekea miaka 15 ya huduma mbalimbali wanazozitoa za kiafya Afrika huku ikiahidi kuendeleza mashirikiano ili kuboresha afya za Watanzania. 
Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti kutoka India ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Shalby  Dk Vikram Shah wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Dk Shah amesema timu ya madaktari bingwa kutoka katika hospitali imekuwa ikija Afrika na kufanya kambi za upasuaji mbalimbali ikiwapo upasuaji wa magoti na nyonga. Amesifu ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na India na kusisitiza kuendelea kusaidiana katika shughuli zao ili kuboresha afya na maisha ya wananchi wa pande zote mbili. 
 “Tanzania na India zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na kambi za kimatibabu mbalimbali zinazofanywa na madktari wa Shalby nchini na Afrika kwa ujumla ni kithibitisho cha utu na upendo baina ya India na Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Dk Shah. 
 Dk Shah ambaye anaaminika kuwa daktari aliefanya upasuaji wa kubadilisha magoti mara nyingi zaidi, ambapo mpaka sasa ashafanya upasuaji zaidi ya 85,000, alisema teknolojia ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya na kuahidi kuboresha zaidi mashirikiano na Tanzania.
Dk Vikram Shah akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria halfa hiyo
Daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Shalby kutoka nchini India, Dk Vikram Shah akifurahia jambo na  Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Phili Mangula (katikati) pamoja na Dk Edmund Mndolwa (kushoto) katika halfa ya kusherekea miaka 15 ya huduma za hospitali hiyo barani Africa iliyofanyika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni


Baadhi ya wshiriki waliohudhuria hafla hiyo.
Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.