NA LUGENZI KABALE

AKIITIKIA agizo la Rais John Pombe Magufuli alilowataka wateule wake kuwa wabunifu na kujituma ili kuwaondolea wananchi shida mbalimbali , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametatua migogoro takribani 8, 000 iliyowahusisha zaidi ya watu 80, 000 ndani ya takribani miezi minane kati ya Disemba mwaka jana na Mwezi Juni mwaka huu.

Makonda ametekeleza jukumu hilo kupitia timu ya wanasheria 35 wanaojitolea kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kiongozi wa timu ya Wanasheria hao, Georgia Kamina, aliitaja baadhi ya migogoro ambayo timu yake imekuwa ikisuluhisha kupitia Ofisi za Wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile ya umiliki wa ardhi na michakato ya mirathi mahakamani na katika ngazi ya familia,

Migogoro mingine ambayo timu hiyo ya wanasheria imekuwa ikimsaidia Makonda kuitatua kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya ya Ilala (Sofia Mjema), Kinondoni (Ally Hapi), Temeke ( Felix Lyaniva ), Ubungo (Kisare Makori ) na Kigamboni (_Hashimu Mgandilwa ) ni pamoja na ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika, ajira na mikataba ya ajira, ubakaji, faili kupotea mahakamani, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, umiliki wa nyumba, umiliki au mauziano ya ardhi, mikopo kutoka mabenki ya biashara, uuzwaji mali mbalimbali kwa kukiuka sheria au makubaliano na hata ukosefu wa uaminifu.

Akiiongea kwa niaba ya Makonda, Kamina aliliambia Habari LEO katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alitaja migogoro wanayopokea na inayotia fora katika mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile inayohusisha masuala ya mirathi, umiliki wa ardhi, ajira na mikataba kati ya waajiri na waajiriwa, ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika na baadhi ya wananchi kuingia mikataba mibovu na mabenki katika harakati za kupata mitaji ya biashara.

"Mheshimiwa Paul Makonda alichukua jukumu la kuanzisha huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi kutokana na uzoefu alioupata katika ziara ya kukutana na wananchi aliyofanya mkoa mzima mwezi Novemba mwaka jana," alibainisha Kamina na kuongeza kuwa ili kuwaepusha wananchi na mchakato mrefu na unaoumiza wa kumaliza migogoro yao mahakamani aliamua kuunda timu ya wanasheria wa kujitolea ili kutekeleza dhamira hiyo ya kuwasaidia wananchi wenye migogoro mbalimbali ya kisheria.
Kiongozi wa timu ya wanasheria hao aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Mkoa aliguswa na namna baadhi ya wananchi walivyokuwa wakipoteza mashamba, nyumba, mali na hata kufukuzwa kazi kwa uonevu kwa kukosa uelewa wa sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...