Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna  Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia  Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu  wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya  Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...