THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

IGP SIRRO AKUTANA NA BAADHI YA MAKAMANDA AKIWA SAFARINI MIKOA YA KANDA YA ZIWA

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora Magiligimba, IGP Sirro amepita mkoani Singida, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiweka saini katika kitabu cha wageni katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, na kuzungumza na baadhi ya askari na maofisa (hawapo pichani), IGP Sirro, amepita katika wilaya hiyo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Manyoni (OCD) Cleophace Magesa, IGP Sirro, amepita katika wilaya hiyo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akifurahia jambo na kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro J. Muliro, IGP Sirro, amepita mkoani humo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo. Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi