Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Bw. Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akisikiliza maelekezo ya jinsi linavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru Bw. Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam
 Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya kichina.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu(watatu kushoto), baada ya makabidhiano ya magari manne kutoka kwa kampuni hiyo ikiwa ni mchango wao katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini.Wengine ni viongozi wa juu wa jeshi na viongozi wa kampuni ya Haval.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay, jijini Dar es Salaam. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...