THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Ivomapunda Sports Centre yaandaa kliniki maalumu kwa makipa wote na makocha wa magolikipa Julai 14, 2017 uwanja wa Karume jijini Dar es salam

Kipa wa kimataifa mstaafu wa Taifa Stars Ivo Mapunda ameandaa clinic ya magolikipa siku ya tarehe14  Julai, 2017  itayofanyika katika uwanja wa Karume kuanzia saa mbili asubuhi.  Kituo  cha Ivomapunda Sports Center ndio kimeandaa hii clinic.
Mgeni rasmi ni mkufunzi anayetoka Taasisi ya michezo ya Keepers Foundation nchini Poland, Marek Dragozs. 
Hivyo  makipa wote na makocha wa magolikipa wanaalikwa kuhudhuria kwa mchango mdogo wa shilingi 5000 tu. Hii si ya kukosa!