Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka watumishi wa halmashauri ya mji wa Tarime na Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea. 

Jafo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hizo mbili wakati wa ziara yake leo wilayani Tarime mkoani Mara.

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kutembelea miradi ya afya, elimu, daraja na ujenzi wa nyumba za watumishi.

Jafo ameiagiza viongozi wa halmashauri hizo mbili kukaa na kufanya maamuzi ya majengo ya halmashauri ya wilaya ya Tarime yaliyopo ndani ya eneo la halmashauri ya mji yatumike kwa matumizi ya kiofisi ya halmashauri ya mji.

Aidha ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri ya mji zihamishiwe halmashauri ya wilaya ili waende kuanza ujenzi wa ofisini katika eneo lao badala ya kukaa ndani ya eneo la halmashauri mji.

“Kitendo hichi kinawakosesha wananchi haki yao ya kupata huduma kwa ukaribu jambo ambalo ndilo lilikuwa msingi wa kugawa halmashauri hizo,”amesema Jafo

Naibu Waziri Jafo amemaliza ziara yake na kuelekea wilaya ya Rorya, mkoani Mara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea eneo la mapokezi la hospitali ya Tarime na kuagiza lijengwe banda kwa ajili ya kukaa wananchi badala ya kukaa juani kama ilivyo hivi sasa. 
Watumishi wa Halmashauri mbili za Tarime wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Majengo yaliyojengwa na wadau wa mgodi wa North Mara kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Tarime. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...