Na Faki Mjaka - MAELEZO,  Zanzibar
Mji wa Drewits uliopo Jiji la Potsdam nchini Ujerumani kwa kushirikiana na Shehia ya Kikwajuni Juu wamesaini hati ya makubaliano ya Mradi wa mahusiano mema baina ya Jiji la Potsdam na Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Miongoni mwa Vipengele vya makubaliano hayo ni kuijenga miundombinu ya Majumba ya Mjerumani Kikwajuni ili kuhakikisha muonekano wake inafanana na Mji wa Drewits wa Potsdam Ujerumani. 
 Akizungumza katika Hafla hiyo Meya wa Jiji la Potsdam Jann Jakobs amesema amefurahi kuona mambo mbalimbali yameanza kutekelezwa kabla ya utiaji saini jambo ambalo linaonesha matumaini mazuri. 
Miongoni mwa mambo ambayo yameanza kutekelezwa ni pamoja na upandaji Miti inayozunguka Uwanja wa Mnazi mmoja na Mtaro wa kutirishia Maji machafu katika eneo hilo. Meya huyo amesema atahakikisha mradi huo unafikia malengo yake kwa ajili ya maslahi mapana ya Watu wa Ujerumani na Zanzibar kwa ujumla.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam nchini Ujerumani Mhe. Jann Jakobs akikagua Mti alioupanda Mwaka 2014 alipotembelea Zanzibar mwaka huo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam nchini Ujerumani  Mhe. Jann Jakobs na Ujumbe wake wakipita katika Maeneo ya Kikwajuni kwa Mjerumaini kabla ya hafla ya kusaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema baina ya Jiji la Potsdam na Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wananchi wa Shehiya ya Kikwajuni Juu wakisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam Ujerumani Mhe. Jann Jakobs mara baada ya kutembelea maeneo ya Kikwajuni kwa Mjerumani. 
 Sheha wa Shehiya ya Kikwajuni juu Mzee Juma Saadat Haji na  Kati Anton Mkurugenzi wa Nyumba za kulelea Watoto wa Drewtz wakisaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema Baina ya Mji wa Drewits na Kikwajuni Mjini Zanzibar kulia yao ni  Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam Ujerumani Mhe. Jann Jakobs 
Picha ya Pamoja ya Wananchi wa Kikwajuni na Ujumbe kutoka Jiji la Potsdam mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema Baina ya Mji wa Drewits na Kikwajuni Mjini Zanzibar Picha na Makame Mshenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...