Na Tiganya Vincent-RS_TABORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kesho tarehe 23 Julai 2017 ,anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani hapa kwa ajili ya uzinduzi wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisi kwake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema Mhe. Rais Dkt.Magufuli atawasili mkoani Tabora akitokea Kigoma ambapo wanatarajia kumpokea katika Wilaya ya Kaliua siku ya Jumapili .

Alisema kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Kaliua kuzindua uzinduzi wa barabara kutoka Kaliua hadi Kazilambwa na baadaye atapata fursa ya kuwahutubia wananchi.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa akiwa njiani kuelekea Tabora Mhe Rais Magufuli atazinduza barabara ya Urambo hadi Tabora siku hiyo hiyo na ambapo pia atawahutubia wakazi wa Urambo na kisha kuelekea Tabora.

Alisema kuwa siku ya Jumatatu Rais ataweka Jiwe la Msingi ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuja katika miji ya Nzega , Igunga na Tabora na baadae kuzindua upanuzi na ukarabati wa njia za kurikia Ndege katika Uwanja wa Tabora.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa siku hiyo hiyo ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atazindua barabara ya Tabora hadi Nzega na ile ya Tabora hadi Nyahua na mchana atawahutubia wakazi wa Tabora katika Viwanja vya Chipukizi.

Alisema ujio wa Rais Magufuli kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora ni sawa na usemi usemao Mgeni Njoo Mwenyeji Apone kwani zara yake mkoani hapa inazidisha matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na jirani zake ya kuendelea kufunguka milango au fursa mbalimbali za uchumi baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya miundo mbinu.

Bw. Mwanri alitoa wito kwa niaba ya wananchi wa Tabora kuwakaribisha wananchi kujotokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...