Na Dotto Mwaibale

 SERIKALI imeahidi kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika sekta ya utalii hususani kwenye utungaji wa sera pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya uendeshwaji wa shughuli hizo nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Utalii Tanzania, Denis Simkoko katika hafla fupi ya uwasilishwaji wa Ripoti ya Utalii Tanzania kwa mwaka 2017 kutoka kwa Jumia Travel, kampuni inayojishughulisha na huduma za hoteli na usafiri mtandaoni tukio lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.

“Bila shaka mafanikio tuliyonayo kwa sasa katika sekta ya Utalii nchini ni matokeo mazuri ya ushirikiano wa karibu baina ya serikali na wadau wengine. Shirikisho la Utalii Tanzania lipo kama daraja katika kuwaunganisha wadau mbalimbali wa sekta hii nchini kote na wizara husika yenye mamlaka kwa mujibu wa serikali. 

Huwa tunakutana na wadau wa utalii ambapo ni takribani vyama 12 nchini kote ndani ya kipindi maalumu cha mwaka na kujadili masuala mbalimbali yanayotukabili. Baada ya hapo sasa ndiyo sisi kama shirikisho huwa tunayawasilisha maoni hayo kwa serikali ili kupata ufumbuzi na pia kutengeneza fursa ambazo zitatukutanisha pamoja wadau katika meza moja ya majadiliano, “ alisema  Simkoko.  

“Mbali na mchango wetu kwenye kupendekeza maboresho ya kodi na sera, pia tunao watu wetu kwenye vikosi kazi na kamati mbalimbali ambao hufanya kazi kwa ukaribu na serikali. Ingawa bado kuna changamoto katika kupata ushirikiano kamili au wa moja kwa moja baina ya serikali na sekta binafsi, bado tunaimani juu ya mifumo thabiti na ya uwazi katika uandaaji na ufanyikaji wa mikutano, majadiliano na mafunzo. 
 Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee, akizungumza katika hafla fupi ya uwasilishwaji wa Ripoti ya Utalii Tanzania kwa mwaka 2017 kutoka katika kampuni hiyo inayojishughulisha na huduma za hoteli na usafiri mtandaoni tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
 Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Geofrey Kijangwa akizungumza kwenye hafla hiyo.

Maofisa wa Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT),  wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho hilo, Denis Simkoko, Meneja Mkuu wa Mauzo wa Hoteli ya Ramada Resort Dar es Salaam, Amina Kapya na Ofisa Tawala wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli  Tanzania (HAT), Jeniffer Abel.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...