THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

JWTZ KUKABIDHI MAJENGO WILAYA YA MISENYI


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                      DAR ES SALAAM, 11 Julai, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kukabidhi Majengo ya kituo cha afya Kabyaileishozi,kituo cha malezi ya Wazee cha kilima na shule ya sekondari ya Omumwami yaliyoko wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera tarehe 12 Julai 2017 kuanzia saa mbili kamili asubuhi 2:00.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu SSera,Uratibu na Bunge Mhe Jenista Mhagama.

Ukiwa mdau wa habari inaombwa kutuma mwakilishi wa chombo chako cha habari ili kufanya coverage la tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.Natanguliza shukrani.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Rommel Mauma Anasema:

    JWTZ, acheni kutumia baruapepe ya yahoo.com/