THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KADA WA CCM LAWRENCE MABAWA AANZISHA KAMPENI YA MAGUFULI BAKI

Na Humphrey Shao-Globu ya Jamii.

Kada wa chama caha Mapinduzi (CCM) kutoka wilaya ya Sengerema Lawrence Mabawa ametangaza kampeni yake mpya itakayo kwenda kwa jina la 'MAGUFULI BAKI'.

Mabawa amesema kuwa Kama jinsi Watanzania na wasio Watanzania tunavyotambua kazi kubwa na nzuri ya kutetea na kupigania rasilimali za Taifa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa wananyonge na masikini wa Watanzania wote bila kujali jinsia, dini,kabila, kuchukuwa jukumu la kumpongeza na kumtia moyo Rais na Serikali yake na si kumkatisha tamaa.

" Mimi kama Mtanzania mzalendo na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nimeamua kuchukuwa jukumu la kuanzisha kampeni ya ‘Magufuli Baki’ yenye lengo kumpongeza Rais kazi anayoifanya bila kujali itikadi zao. 

Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha Mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wanafunzi wa Sekondary na wananchi kwa kufanya mikutano yenye nia njema ya kumwomba Mhe. Rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea Watanzania wanyonge na masikini"Amesema Mabawa.

Amesema kuwa Kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kupitia mikutano tutakayoifanya ambapo wataweza kutoa maoni kuhusu utendaji wa serikali kwa ujumla ikiwa ni kupongeza na hata kukosoa.

ametaja kuwa hili kukamilisha kampeni hii tutatumia Kurasa za Mitandao ya Kijamii maalum ambazo zimeandaliwa kwa kampeni hiyo ambapo tutaweka maoni na pongezi za kila mshiriki wa kampeni hiyo. Mbali na kutumia mitandao ya kijamii tutashirikiana bega kwa bega na vyombo vya habari pamoja na wanahabari kufanikisha kampeni hii.

Ameongeza kuwa lengo la kampeni hii mbali na kompongeza Mhe. Rais na Serikali yake pia tutapata fursa ya kuwasikiliza wananchi moja kwa moja ili kugundua ukweli halisi kutoka kwao wa namna gani wanaona utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa akizungumza na waandishi wa haabri juu ya kampmeni yake ya Magufuli baki ambayo ameitambulisha kwa Wanahabari kuhusu kuanza kampeni ya kumshinikiza Rais Magufuli aendelee kusimamia misimamo yake katika kuongoza nchi na kuacha kuyumbishwa na maneno ya kwenye mitandao
Afisa Habrai Idara ya Habari MAELEZO , Georgina Misama akimtambulisha Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa kwa Waandishi wa Habari.
Sehemu ya Waandishi walioshiriki mkutano huo wakimsikiliza Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa kwa makini