Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kimeweka kambi katika Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti.


Kocha mkuu wa timu hiyo Mecky Mexime amejumuisha kikosi cha zamani na wale wa watakaoungana na wenzao katika kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya.

Katika sura mpya za kikosi cha Kagera Sugar ni Juma Nyoso aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutokujihusisha na soka, Omary Daga na Abdala Mguhi kutoka African Lyon iliyoshuka daraja.



 Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .
Dakatri wa timu ya Kagera Sugar akiganga mchezaji aliyeumia katika  mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

Kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wanaoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es salaam.Picha na Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...