Na Greyson Mwase, Kagera 

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema vijiji na vitongoji vyote vya mkoa wa Kagera vinatarajiwa kupata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2021 kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) 

Dkt. Kalemani aliyasema hayo mapema Julai 11, 2017 kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) utakaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera pamoja na kumtambulisha mkandarasi atakayefanya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya mradi katika mkoa huo. 

Alisema utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Kagera utahusisha vipengele vitatu ambavyo ni pamoja na kusambaza umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme na kuongeza wigo wa usambazaji umeme katika vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya maeneo na vitongoji havikuungwa. 

Waziri Kalemani alisema kipengele cha tatu kinahusisha usambazaji wa umeme utokanao na vyanzo vya nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi hususan visiwani. 

Aliendelea kusema kuwa utekelezaji wa mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 141 kwa gharama ya shilingi bilioni 45.43 na kuongeza kuwa utekelezaji wa sehemu ya kwanza ulianza tangu mwezi Februari mwaka huu ambapo inatarajiwa kukamilika mapema Aprili, 2019 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata  utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa. Kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa. Kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga na kushoto ni Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate. 
Waliosimama ( kuanzia wa pili kutoka kulia mbele), Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt. Gideon Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji wa Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika kijijini hapo mapema Julai 11, 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...