Na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania.

5/07/2017

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, amesema kwamba Mahakama ya Tanzania imejipanga kusikiliza kesi zilizokwama zinazohusu mabenki kwamba ili ziweze kwenda kwa haraka na kulingana na sera ya, ikiwemo kuwezesha ukuzaji wa uchumi wa nchi .

Kauli hiyo ilitolewa na jana Kaimu Jaji Mkuu huyo , wakati alipotembelea Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko, Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumzia kuhusu mlundikano wa kesi mahakamani alisema Mahakama ya Tanzania inafanya mikakati ya kuweza kuzipunguza.

“ Tunahitaji majaji zaidi ya 30 ili kuweza kupunguza mlundikano uliopo wa kesi zilizopo Mahakamani,” alisema Profesa .

Profesa Juma alisema hayo, baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho, ambapo alisema Mahakama ya Tanzania, imepiga hatua katika mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), akitolea mfano Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, ambapo alishauri kwamba mahakama zingine za chini ziweze kujifunza.

Profesa Juma pia alitoa ushauri kwa watu wenye viwanda nchini kufuata sheria na taratibu, waweze kusajiliwa kwa kuwa kufanya hivyo kutawafanya washiriki kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi wa nchi .

“ Nimetembelea Banda la Mkemia Mkuu wa Serikali nimeona mazao na bidhaa mbalimbali,hivyo ni vema watu wanaotengeneza bidhaa wakasajiliwa ili waweze kufuata sheria na taratibu za nchi, kwa kuwa kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zao kuwa bora na wataweza kuiwezesha nchi kushiriki katika uchumi wa kisasa,” alisema Profesa Juma.

Katika maonesho hayo, Kaimu Jaji Mkuu huyo, miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea banda la Mahakama ya Tanzania, Jeshi la Magereza , Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),banda la Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikal(GCLA)i, banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA). Banda la Wakala wa Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA) Mamlaka ya Reli Tanzania, na Mabanda la Mamlaka ya Reli Tanzania, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ,Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC .
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika katika banda la Mahakama sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Aliyesimama mwenye miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu
Mhe. Edson Mkasimongwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...