THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAIMU KAMISHNA USTAWI WA JAMII ATEMBELEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BWENI LA WAZEE NA MRADI WA MAJIKO YA GESI KATIKA MAKAZI YA KULEA WAZEE YA KOLANDOTO SHINYANGA

Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe jinsi ya kuwasha Jiko la Gesi lililopo katika kituo hicho ikiwa ni moja ya mradi wa majiko ya Gesi katika Makazi ya kulea wazee nchini wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Rashid Mfaume.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(Kushoto) akiangalia moja ya jiko linalotumia Nishati ya Gesi linalowaka wakati alipotembele kukagua maendeleo ya mradi huo hivi karibuni.
Muonekano wa Majiko yanayotumia Nishati ya Gesi yatakayotumiwa kuhudumia katika makazi ya kulea wazee ya Kolandoto na makazi mengine ya kulea wazee nchini.