KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia. 
Hayo ameyazungumza jana Jijini Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao.
Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji wa pande zote. 
Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari. 
“Yapo malalamiko mengi ya utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi 1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti zao tuweze kuwalipa”Alisema.

KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao. Kushoto ni Maneja wa Mawasilino TPA Janeth Ruzangi.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...