THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Na Robert Hokororo

Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata za Lagana, Itilima na Talaga. Katika ziara hiyo wajumbe hao pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwadulu iliyopo kata ya Lagana.

Wakiwa eneo hilo wajumbe hao kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri, Boniphace Butondo walipongeza juhudi za uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu na kutumia vizuri fedha za Serikali.

Butondo aliwataka wanakamati ya shule kuendelea kuupa ushirikiano uongozi wa shule hiyo ili waendelee kushughulikia shughuli za maendeleo kupitia mpango wa elimu bure. Kamati hiyo iliweza pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Lagana ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi ambapo walihimiza waendelee kuchangia.

Ziara hiyo pia ijumuisha kata ya Itilima ambapo wajumbe na wataalamu hao walikagua ujenzi wa vyumba viwili vya darasa shule ya msingi Ipililo pamoja na kata ya Talaga ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Nhobola.

Waliridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo walimpongeza afisa elimu ufundi, Moshi Balele kwa kufuatilia kwa ukaribu shughuli zote zinazoendelea.

Hiyo ni mojawapo ya ziara za kukagua miradi ya maendeleo zinazofanywa na kamati mbalimbali za Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiongozana na mchumi kutoka halmashauri hiyo, Veronica Massawe katika kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiwaelekeza jambo mafundi waliokutwa na kamati wakiendelea na shughuli ya kusakafia mojawapo ya vyumba vya madarasa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa mojawapo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lagana wakati wa ziara hiyo.
Ofisa elimu ufundi, Moshi Balele akiwaelekeza wajumbe wa kamati namna ujenzi wa chumba cha darasa unavyoendelea katika shule ya msingi Ipililo.
Chumba cha darasa katika shule ya msingi Mwamadulu ata ya Lagana kikiwa katika hatua mwisho wa ujenzi wake.