THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAMPUNI ZA PUMA, TIPPER NA TPB ENERGY ZATOA GAWIO KWA SERIKALI SH. BILIONI 7

SERIKALI imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye kutatua changamoto za Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na biashara ya mafuta.
Akikubali ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.
Pia alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.
Awali kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.
Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi
Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.

KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA