THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI.

Na Erasto Ching’oro WAMJW.

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao  kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na  kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.

Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.

“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
  Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA