THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KUHITIMISHWA KWA AWAMU YA PILI YA UREJESHAJI HALI YA MIUNDOMBINU YA SERIKALI MKOANI KAGERA BAADA YA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI SEPTEMBA, 2016.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, kama ishara ya kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimshuhudia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, wakati wa  kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi, Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo,  (katikati) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).