Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

Mlalamikaji katika kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk.William Morris dhidi ya Mchungaji Joseph Mwingira na Philis Nyimbi amewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiomba, mkewe, Mwingira na Mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.
Maombi hayo ya Dr. Morris yamewasilishwa mahakamani hapo leo na wakili wake Respicious Ishengoma mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Katika Maombi hayo Dr. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.

Katika madai yake, Dkt. Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).Mapema mahakamani hapo, wakili Ishengoma aliomba mahakama ianze kusikiliza maombi hayo kabla ya kuingia kwenye kesi ya msingi lakini Wakili wa Mchungaji Mwingira na Dk. Phillis waliomba kupatiwa muda ili waweze kuwasilisha majibu yao.
Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 2, mwaka huu. 
Katika maombi, yake Dk. Morris, anaiomba mahakama itoe amri kwake yeye, walalamikiwa Mchungaji Mwingira na Dk. Phillis pamoja na mtoto waende kupimwa DNA.
Desemba 28, 2011 Dk. Morris na Phillis walifunga ndoa katika Kanisa la Anglican, Upanga na wakati wa ndoa yao (Mchungaji Mwingira na Phillis) waliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kubahatika kupata mtoto mwenye miaka tisa na matatizo mbalimbali ya kiafya kwa mkewe.

Mlalamikaji huyo anadai alitoa taarifa polisi katika kituo cha Kibaha, ambapo aliambiwa ni suala la uzinzi au udhalilishaji ambalo haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa afungue kesi ya madai.
Amedai kitendo cha mkewe kuwa na uhusiano na Mwingira kimeharibu mipango yake ya mbele kiasi cha kumfanya apoteze matumaini ya kuishi.
Aidha, kitendo hicho kimemuaibisha na kushusha hadhi yake ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...