MFANYABIASHARA mdogo wa kuuza duka Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Leonard Bagumako, amekumbwa na mafuriko ya mamilioni kutoka bahati nasibu ya Biko, baada ya kutangazwa kushinda Sh Milioni 20 za droo ya 26 iliyochezeshwa leo.

Bagumako aliibuka kidedea ikiwa ni siku chache baada ya donge nono kama hilo katika droo ya 25 kwenda kwa Ally Hassan Lukinga wa Mtwara.

Akizungumza saa chache baada ya kupatikana mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles, alimpongeza Bagumako kwa kuibuka mshindi kwenye droo hiyo ya aina yake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya uwapo wa Biko kutajirika.

Alisema biko ni mchezo rahisi unaotoaa ushindi wa zawadi za fedha za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka Jumatano na Jumapili.

“Kila mtu anaweza kuibuka na shangwe kutoka Biko kwa kutwaa Sh Milioni 20, ambapo kucheza biko ni rahisi kwa sababu inachezwa kwa simu za mikononi ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa wachezaji kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea, ambapo Sh 1000 ina nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye kuwania sh Milioni 20, huku namba ya kampuni ya Biko ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwataka Watanzania wote kuuamini mchezo wa Biko kwa kwakuwa umekuwa ukiendeshwa kwa kuzingatia kanuni na sheria walizokubaliwa na nchi yetu.
“Biko ni mchezo ambao kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja na mamilioni ya mwisho wa wiki, hivyo nawaomba wacheze kwa kujiamini maana unafuata kanuni zote,” Alisema.

Naye mshindi huyo wa Sh Milioni 20 kutoka Kigamboni, Leonard Bagumako, alipokea ushindi huo kwa furaha, ingawa alisisitiza kuwa bado haamini kama ni yeye aliyepigiwa simu ya kupewa taarifa za ushindi.

“Ndio mimi huyu huyu unayesema nimeshinda Sh Milioni 20 za Biko” alisema Bagumako huku akisisitiza kwamba amekuwa mchezaji mzuri wa Biko kwa muda mrefu.

Kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, mchezo wa Biko umeshakabidhi zaidi ya Shilingi Bilioni moja kutoka kwa washindi wao katika mikoa mbalimbali, ikiwa ni mwelekezo mzuri wa uwapo wa mchezo huo wa Biko Tanzania.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki kushoto akiandika kumbukumbu muhimu baada ya kumpata mshindi wa droo ya 26 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo Leonard Bagumako aliibuka kidedea kwa kujizolea Sh Milioni 20. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...