Timu ya wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) wameanza maandalizi ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Umeme Vijijini Awamu yaTatu (REA III) katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Simiyu. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani mapema wiki ijayo. Sambamba na uzinduzi huo, wakandarasi watakaotekeleza mradi huo watatambulishwa kwa wabunge, madiwani na wanakijiji kutoka katika mikoa husika ambapo miradi itatekelezwa.
 Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwenye eneo la jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambalo liko katika hatua za mwisho wa ukamilishwaji wake.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Mhe. Diwani Athuman (mbele) akizungumza na timu  ya watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) na wakandarasi ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu, Shaban Lissu (katikati) akisalimiana na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Elineema Mkumbo (kulia) mara baada ya  timu ya maandalizi kuwasili katika eneo la Rwabigaga wilayani Kyerwa ambapo kutafanyika uzinduzi huo kwa mkoa wa Kagera
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (kushoto) akielezea miradi ya umeme vijijini  inayotekelezwa na Wakala huo. Kulia ni Meneja Mipango Miradi na  Tafiti kutoka wakala huo,  Mhandisi Jones Olotu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...